MKURUGENZI AZINDUA MAJENGO MAPYA YA HOSPITAL YA KITENGO CHA KUSAFISHA FIGO, MENO NA WATOTO NJITI
- Peramiho Hospital
- Jul 30, 2024
- 1 min read
Updated: Oct 5, 2024
Mnamo tarehe 15 mei 2021 Mkurugenzi wa hospital ya mtakatifu Joseph Peramiho Dr Ansgar Stufe OSB alifungua majengo mapya katika hospitali ya mtakatifu Joseph Peramiho ambayo ni majengo ya idara ya meno, maabara, jengo la wodi za watoto njiti, jengo la kusafishia figo (Hemodialysis) na mradi wa maji. Uzinduzi huo uliambatana na uongozi wa Wilaya ukiongozwa na mkuu wa wilaya ya Songea Vijijini ndugu Kamando Mgema. Uzinduzi wa majengo hayo ni hatua kubwa ya maendeleo katika hospitali na muendelezo wa uboreshaji wa huduma za Afya katika hospitali ya mtakatifu joseph Peramiho.





