HOSPITALI YA ST. JOSEPH PERAMIHO YAANZA KUTOA HUDUMA YA CT SCAN
- Peramiho Hospital
- Nov 10, 2024
- 1 min read
Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Joseph PERAMIHO imeanza kutoa Huduma ya Upimaji Magonjwa mbalimbali kwa kutumia Teknolojia za Kisasa .Akizungumza katika hafla ya Kuzindua mashine hiyo ya CT-Scan ,Mganga Mkuu wa Hospitali Mtakatifu Joseph PERAMIHO Dkt.Adeodas Haule amesema kuwa , Mradi huo umekamilika na ulianza kutoa Huduma Tangu Mwezi Septemba,2024 baada ya kukaguliwa na Wataalamu kutoka Tume ya Mionzi (Taec) ambapo hadi Mashine hiyo imehudumia Wagonjwa 70 wenye shida mbalimbali. Hospitali ilipokea Fedha kutoka kwa wafadhili wamissionari wa Benedict kiasi cha Shilingi milioni mia mbili na kumi na Nne elfu ,kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la CT-Scan, na Baada ya jengo kukamilika Wafadhili hao walinunua Mashine ya CT-Scan ambayo iliyogharimu Shilingi Bilioni Moja na Milioni Mia Tano Hamsini."Adam Mlele ambae ni Afisa Tawala wa Wilaya ya Songea amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas ambapo amempongeza Mkurugenzi wa Hospitali hiyo ya St.Joseph PERAMIHO Dkt. Ansgar Stufer pamoja na Menejimeti Nzima ya Hospitali hiyo kwa kuwezesha kupatikana kwa mashine ya CT-Scan .Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa Juhudi zote ambazo amekuwa akizifanya katika kuhakikisha Sekta ya Afya inaendelea kuimarika na Wananchi Kupatiwa matibabu Bora





